Safari Forums
Karibu kwenye mtandao wa jamii, ni bure kabisa kuutumia ILA kabla ya ku post topic yeyote au ku comment unatakiwa kujisajili.

Ni rahisi sana tunachohitaji ni kuandika email yako na username tu.


 
HomeHome  FAQFAQ  SearchSearch  RegisterRegister  Log inLog in  

Share | 
 

 Vita vya kugombea madaraka Bunda

Go down 
AuthorMessage
Admin
Admin
avatar

Posts : 100
Points : 310
Reputation : 0
Join date : 2012-06-04

PostSubject: Vita vya kugombea madaraka Bunda   Wed Jun 20, 2012 6:35 am

Tuesday, 19 June 2012 21:35

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira na Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Esther Bulaya, juzi walizozana katika kile kinachoonekana kuwa ni kuwania madaraka katika Jimbo la Bunda mkoani Mara, katika uchaguzi mkuu 2015.

Sakata hilo lilitokea nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kuahirishwa kwa kikao juzi usiku, ambapo Wassira alimfuata Bulaya na kumhoji kwamba kwanini alitoa maneno ya kuipinga bajeti ya Serikali.

Wassira ambaye pia ni Mbunge wa Bunda (CCM) alimwambia Bulaya: “Mimi ndiye Mbunge wa Bunda, wewe huwezi kujifanya ndiye uliyetumwa na wananchi kuja kusema maneno ya uwongo hapa, eti unaipinga bajeti ya Serikali, ni nani aliyekutuma?”

Waziri huyo alikwenda mbali na kumwambia mbunge huyo kijana kwamba, “wewe tunakufahamu una pande mbili (upinzani na CCM) na kila siku unashirikiana na Halima Mdee (Kawe-Chadema), tunakujua kwamba uko CCM na Chadema.”
Back to top Go down
http://safari.darkbb.com
 
Vita vya kugombea madaraka Bunda
Back to top 
Page 1 of 1
 Similar topics
-
» Produser Senran Kagura Kerjakan Game Vocaloid IA untuk PS Vita

Permissions in this forum:You cannot reply to topics in this forum
Safari Forums :: General Forums :: Jukwaa la Siasa-
Jump to: