Na Gadi Solomon
TUSIKUBALI. Inafaa Watanzania tutambue kwamba lugha ni sehemu ya utamaduni unaoweza kulitambulisha taifa letu nje ya mipaka yetu.
Ndiyo maaana kumekuwapo na Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita) linalosimamia na kuratibu mambo mbalimbali yanayohusiana na lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Tanzania.
Ieleweke wazi kwamba chombo hiki kinafanya kazi ya umma na siyo kwa ajili ya wasomi peke yao kama wengi wanavyodhani.
Miaka ya hivi karibuni kumekuwapo na mwamko wa mashindano haya maarufu kama Miss Tanzania ambayo mwaka huu yanafahamika kama Redd’s Miss Tanzania ambayo kwa sasa yamejitanua zaidi katika ngazi ya vitongoji.
Soma zaidi
HAPA