Bukoba ni mji nchini Tanzania ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Kagera. Eneo la mji ni wilaya ya Bukoba mjini. Kulingana na sensa ya mwaka 2002 idadi ya wakazi wake ilihesabiwa kuwa 81,221.
Bukoba iko kando la Ziwa Viktoria Nyanza upande wa magharibi. Mji ulianzishwa kuanzia 1890 wakati Wajerumani waliteua sehemu hii kwa boma la jeshi lao la kikoloni na kuifanya makao makuu ya mkoa.
Kata za Bukoba Mjini
Bakoba | Bilele | Buhembe | Hamugembe | Ijuganyondo | Kagondo | Kahororo | Kashai | Kibeta | Kitendaguro | Miembeni | Nshambya | Nyanga | Rwamishenye