Wilaya ya Muleba ni wilaya moja ya Mkoa wa Kagera. Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 386,328.
Muleba ilikuwa tarafa ya Bukoba ikaanzishwa kama wilaya ya pekee mwaka 1984. Makao makuu yako kwenye mji wa Muleba uliokuwa na wakazi 10,000 wakati wa sensa 2002.
Wilaya ina tarafa tano za Muleba, Kimwani, Nshamba, Izigo na Kamachumu. Eneo la wilaya ni kilomita za mraba 3,444 pamoja na 7925 km² za maji ya Ziwa Viktoria zikiwa pamoja na visiwa 20.
Kata za wilaya ya Muleba: Tembelea kurasa zake
;;;;;;;;;;;