Wilaya ya Tarime ni wilaya mojawapo ya wilaya za Mkoa wa Mara. Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 492,798. Zamani ilijulikana kwa jina la “Wilaya ya Mara Kaskazini”. Mwaka 2006 sehemu ya mashariki ya Tarime imekuwa wilaya mpya ya Rorya lakini haina makao makuu bado.
Tarime imepakana na Kenya (wilaya za Migori, Trans Mara na Kisii) upande wa kazkazini na mashariki. Hifadhi ya wanyama ya Masai Mara ya Kenya uko upande wa mashariki pia. Upande wa kusini umepakana na wilaya za Musoma mjini, Musoma vijijini na wilaya ya Serengeti. Upande wa magharibi iko wilaya mpya ya Rorya.
Makao makuu ya wilaya yapo mjini Tarime.
Kata za wilaya yaTarime: Tembelea kurasa zake
Binagi | Bumera | Gorong’a | Ikoma (Tarime) | Kemambo | Kibasuka | Manga | Matongo | Muriba | Mwema | Nyakonga | Nyamwaga | Nyandoto | Nyanungu | Nyarero | Nyarokoba | Pemba | Sirari | Susuni | Tarime | Turwa