Wilaya ya Chato ni wilaya mojawapo ya Mkoa wa Geita. Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 251,261 [1] na imekadiriwa kuwa na 318,000 kwa mwaka 2007.
Wilaya hii ilianzishwa mwaka 2007 kutokana na maeneo ya wilaya ya Biharamulo, mkoa wa Kagera, halafu mwaka 2012 ikasogezwa katika mkoa mpya wa Geita.
Kata za wilaya ya Chato: Tembelea kurasa zake
Chato | Bwina | Muungano | Ilemela | Bukome | Katende | Ilyamchele | Muganza | Bwongera | Kachwamba | Kasenga | Ichwankima | Kigongo | Nyamirembe | Buseresere | Bwanga | Nyarutembo | Buziku | Iparamasa | Makurugusi | Butengo | Rumasa.