Mkoa wa Shinyanga ni kati ya mikoa 30 ya Tanzania. Mkoa umepakana upande wa kaskazini na mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera, upande wa kusini na Mkoa wa Tabora. Mkoa wa Kigoma uko upande wa magharibi, na mkoa mpya wa Simiu upande wa mashariki.
Makao makuu yapo Shinyanga Mjini, wenyeji wa mkoa huu ni Wasukuma, Wanyamwezi na Wasumbwa.
Kabla ya kumegwa upande wa mashariki na kuzaa mkoa wa Simiyu ulikuwa na wakazi 2,796,630 kufuatana na sensa ya mwaka 2002, ulikuwa na eneo la kilomita za mraba zipatazo 50,781.
Utawala na Siasa
Wilaya za mkoa wa Shinyanga: Tembelea kurasa zake
1. Kahama 2. Kishapu 3. Shinyanga Vijijini 4 Shinyanga Mjini.
Majimbo ya uchaguzi: Tembelea kurasa zake
1. Shinyanga Mjini 2. Shinyanga Vijijini 3. Kishapu 4. Kahama
Elimu
Shule za msingi zipo 1108 kati ya shule hizo za serikali ni 1092 na shule zisizo za serikali ni 17. Pamoja na shule hizo kuna vituo vya kutolea elimu 1262 kwa watoto walikosa elimu ya msingi MEMKWA.
Kwa mwaka 2008, mkoa ulikuwa na jumla ya shule za sekondari 273. Kati ya shule hizo 255 ni za serikali na shule 18 shule binafsi.
Biashara
Kama ilivyo mikoa mingi ya Tanzania Bara shughuli kuu za kiuchumi za wakazi wa mkoa huu ni kilimo na ufugaji. Mazao makuu ya chakula yanayolimwa ni pamoja na mtama, mahindi, mpunga, mhogo na viazi vitamu. Mazao ya biashara ni tumbaku, pamba, alizeti, karanga na dengu. Shughuli za uchimbaji wa madini ya Almasi pia ni maarufu sana katika mkoa huu, ambazo kwa kiasi kikubwa shughuli hizo zimekuwa zikifanyika katika mgodi maarufu wa Williamson Diamond.
Tembelea
Tovuti rasmi ya Mkoa wa Shinyanga