Mkoa wa Mara ni kati ya mikoa 30 ya Tanzania, Musoma ndipo makao makuu ya mkoa.
Mara imepakana na mikoa jirani ya Mwanza na Shinyanga upande wa kusini, Arusha upande wa kusini-mashariki, Kagera kwa njia ya Ziwa Nyanza (au Viktoria) na Kenya upande wa mashariki.
Idadi ya wakazi ni 1,368,602 (2002) kwenye eneo la kilometa za mraba zipatazo 19,566 ambazo ni sawa na maili za mraba zipatazo 7,554.
Makabila ni mengi kuliko mikoa yote ya Tanzania, kama vile Waluo, Wajita, Waruri, Wazanaki, Wakuria, Wakabwa, Wakiroba, Wasimbiti, Wangoreme, Wakwaya, Waikoma, Wanata, Waisenye, Waikizu, Wasizaki, Wasukuma and Wataturu.
Wilaya za Mkoa wa Mara: Tembelea kurasa zake
1. Bunda 2. Serengeti 3. Tarime 4. Rorya 5. Butiama 6. Musoma Mjini 7. Musoma Vijijini.
Majimbo ya uchaguzi: Tembelea kurasa zake
1. Rorya 2. Serengeti 3. Musoma Mjini 4. Musoma Vijijini 5. Tarime 6. Bunda.
Sehemu kubwa ya Hifadhi ya Wanyama ya Serengeti iko ndani ya Mkoa wa Mara.
Shughuli za kiuchumi katika mkoa huu ni pamoja na kilimo cha mazao ya chakula na biashara kama Pamba, Viazi mviringo na Uvuvi, makao makuu ya mkoa huu yapo mjini Musoma.