Mkoa wa Simiyu ni kati ya mikoa 30 ya Tanzania. Makao makuu yako Bariadi.
Ulianzishwa rasmi Machi 2012 kwa kumega mkoa wa Shinyanga upande wa mashariki.
Kabila kubwa ni lile la Wasukuma.
Uchumi wa Mkoa:
Shughuli kuu za kiuchumi za wakazi wa mkoa huu ni kilimo na ufugaji.
Mazao makuu ya chakula: mtama, mahindi, mpunga, mhogo na viazi vitamu. Mazao ya biashara ni tumbaku: pamba, alizeti, karanga na dengu. Mifugo: inayofugwa ni pamoja na ng’ombe, mbuzi, kondoo, punda, nguruwe na kuku.
Mbali na shughuli za kilimo na ufugaji wakazi wa mkoa huu hujishughulisha na uchimbaji mdogo wa madini, kazi za viwanda na biashara mbalimbali. Viwanda vichache vilivyopo ni pamoja na viwanda vya kuchambua pamba, viwanda vya kusindika mafuta na viwanda vidogo vya ufundi wa fani mbalimbali kama useremala, umakenika, ushonaji wa nguo na viatu.
Utawala na Siasa
Mkoa huu mpya una wilaya tano: Tembelea kurasa zake
1. Bariadi 2. Busega 3. Itilima 4. Maswa 5. Meatu
Mkoa una majimbo saba ya uchaguzi: Tembelea kurasa zake
1. Bariadi Mashariki, 2. Bariadi Magaribi, 3. Maswa Mashariki, 4. Maswa Magharibi, 5. Meatu, 6. Kisesa, na 7. Busega.