Mkoa wa Geita ni kati ya mikoa 30 ya Tanzania. Umepakana na Kagera upande wa magharibi, Shinyanga upande wa kusini na Mwanza upande wa mashariki. Ziwa la Viktoria Nyanza liko kaskazini.
Makao makuu ya mkoa yapo Geita mjini.
Makabila makubwa katika mkoa ndio Wasukuma na Wazinza.
Kabla ya kuanzishwa mkoa mpya wa Geita, ulikuwa sehemu ya mkoa wa Mwanza ambao ulikuwa na wakazi 2,942,148 (sensa ya mwaka 2002) katika wilaya 8 ukiwa na eneo la 19,592 km2.
Wilaya na Siasa
Wilaya za mkoa wa Geita: Tembelea kurasa zake
1. Bukombe 2. Chato 3. Geita 4. Mbongwe 5. Nyang’hwale.
Majimbo ya uchaguzi: Tembelea kurasa zake