Mkoa wa Kagera ni mkoa wa kaskazini-magharibi kabisa katika Tanzani. Jina lake linatokana na Mto Kagera.
Mkoa wa Kagera unapatikana kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania. Makao makuu ya mkoa yapo katika mji wa Bukoba. Mkoa huu unapakana na nchi ya Uganda kwa kaskazini, Rwanda na Burundi kwa upande wa magharibi mkoa wa Kigoma, Mwanza kwa upande wa kusini na ziwa Victoria kwa upande wa mashariki. Mkoa wa Kagera una jumla ya eneo la kilomita za mraba 39,168 kati ya hizo kilometa za mraba 28,513 ni eneo la nchi kavu za kilomita 10,655 ni eneo la maji.
Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002 mkoa ulikadiliwa kuwa na watu 2,033,888. Wakazi wengi wa mkoa huu ni Wahaya, Wahangaza na……
Utawala na Siasa
Wilaya za mkoa wa Kagera: Tembelea kurasa zake
1. Bukoba-mjini 2. Bukoba Vijijini 3. Misenyi 4. Muleba 5. Karagwe 6. Ngara 7. Biharamulo 8. Kyerwa.
Misenyi ni wilaya mpya iliyoanzishwa mwaka 2007 na Kyerwa ikafuata mwaka 2012.
Majimbo ya uchaguzi: Tembelea kurasa zake
1. Bukoba Mjini 2. Bukoba Vijijini 3. Chato 4. Biharamulo Magharibi 5. Biharamulo Mashariki 6. Karagwe 7. Kyerwa 8. Muleba Kusini 9. Muleba Kaskazini 10. Nkenge 11. Ngara
Wakuu wa Mkoa wa Kagera tangu mwaka 1961 ni hawa wafuatao:-
1. Bw. Samuel N. Luangisa (1961 – 1964),
2. Bw. Oswald Marwa (1964 – 1966),
3. Bw. P. C. Walwa (1966 – 1967),
4. Bw. S. S. Semshanga (1967 – 1970),
5. Bw. L. N Sijaona (1970 – 1972),
6. Maj. Gen. Twalipo (1972 – 1974),
7. Brig. M. M Marwa (1974 – 1975),
8. Col.T. A Simba (1975 – 1977),
9. Bw. Mohamed Kisoki (1977 – 1978),
10. Capt. Peter Kafanabo (1978 – 1981),
11. LT.Col. Nsa Kaisi (1981 – 1987),
12. Bw. Horace Kolimba (1987 – 1989),
13. Bw. Paul Kimiti (1989 – 1991),
14. Capt. A. M Kiwanuka (1991 – 1993),
15. Bw. Philip J. Mangula (1993 – 1996),
16. Bw. Mohamed A. Babu (1996 – 1999),
17. Gen. T. N. Kiwelu (1999 – 2006),
18. Col. E. Mfuru (2006 – 2009),
19. Bw. Mohamed A. Babu (2009 – 2011),
20. Col Fabian I. Massawe (2011 hadi sasa
Kwa habari zaidi tembelea,
Tovuti rasmi ya Mkoa wa Kagera