Mkoa wa Mwanza ni kati ya mikoa 30 ya Tanzania. Umepakana na Geita upande wa magharibi, Shinyanga na Simiyu upande wa kusini na Mara upande wa mashariki. Ziwa la Viktoria Nyanza liko kaskazini.
Makao makuu ya mkoa yapo Mwanza mjini.
Wakazi wa mkoa huu ni wa makabila tofauti kati ya hayo kabila kubwa ni Wasukuma hasa upande wa bara, upande wa visiwani ni Wakerewe, na Wakara.
Utawala na Siasa
Kabla ya kumegwa na kuzaa mkoa mpya wa Geita, mkoa wa Mwanza ulikuwa na wakazi 2,942,148 (sensa ya mwaka 2002) ukiwa na eneo la 19,592 km2.
Wilaya za Mkoa wa Mwanza: Tembelea kurasa zake
1. Nyamagana 2. Ilemela 3. Ukerewe 4. Kwimba 5. Magu 6. Misungwi 7. Sengerema
Majimbo ya uchaguzi: Tembelea kurasa zake
1. Nyamagana 2. Ilemela 3. Nyang’hwale 4. Kwimba 5. Sumve 6. Magu 7. Busega 8. Misungwi 9. Buchosa 10. Ukerewe
Mkoa pia unao wabunge watatu(3)wa Viti Maalumu
ELIMU
Mkoa wa Mwanza una jumla ya shule 251 za sekondari, hadi mwaka 2007 mkoa ulikuwa na shule za msingi 1164.
Mkoa wa Mwanza unavyo vyuo vya ualimu 2 vya Serikali ambavyo ni Murutunguru kwa mafunzo ya ualimu wa Daraja A na Butimba kwa mafunzo ya ualimu ngazi ya Diploma. Aidha mkoa una chuo cha ualimu kisicho cha serikali 1 jijini Mwanza kiitwacho Montessori.
Mkoa una chuo kimoja cha ufundi stadi cha serikali ambacho ni chuo cha VETA kilichopo eneo la Nyakato Jijini Mwanza. Aidha kuna vyuo vya ufundi stadi visivyo vya serikali vipatavyo vine. Vyuo vikuu vilivyopo mkoa wa Mwanza ni :-
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania mali ya Serikali.
Chuo Kikuu cha St. Augustine University of Tanzania.
Chuo Kikuu cha TIba – Bugando.
Tembelea
Tovuti rasmi ya Mkoa wa Mwanza
Kama una habari yoyote au ushauri au makala yako kuhusu mkoa huu unaweza kuyapost kwenye kisanduku hapo chini.
Wabeja getegete, wakondya.http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=36639